Header

Wednesday, October 24, 2012

Mnaotumiwa SMS za Cosmic Rays from Mars, soma hapa

Nimetumiwa hiyo TXT mara tatu, ya kuzima simu sababu ya COSMO RAYS,  mara ya tatu sikuzima kwani nilikuwa na kazi muhimu na simu hiyo. Baada ya usiku huo kupita nikaamua kutafuta UKWELI wa fizikia  kuhusu hizi 'Cosmic Rays' au Cosmo wengine wanavoandika. 
Baada ya kusoma niligundua yafuatayo;

  •  Source kuu ya Cosmo kwenye mfumo wa jua na sayari zake ni jua lenyewe na nyota zingine
  • Cosmo ni moja kati ya rays ambazo zinaathiri Ozone (Ozone layer depletion) kwa kifupi uwepo wake unahusishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.
  • Miale ya Cosmo inaongezeka unapopanda katoka usawa wa bahari. kwenda juu, kwahiyo watu wa milimani wanafikiwa na miale hii zaidi
  • Athari za miale hii kwa electonic imeonekana ni kwa vifaa vya kutunza data za computer na vifaa vya ndege na satellite wala sio simu au TV au Redio.
  • Hakuna sehemu nilipoona kuwa Mars inatoa miale hiyo kuja dunian.
  • NASA wanasema, Cosmo zimeongezeka katutokana na kulegea kwa magnetic field ya jua.
Kwa maoni yangu; Kama hizo rays zinatokea huo muda, safari za ndege zingekuwa zinasitishwa na website zote wangekuwa wanafunga mitambo yao kwa muda huo.
Pia nadhani kama watunzi wa hizo SMS wana mpango wa kuendelea, watume message za kututahadharisha kuzima compyuta na sio simu.
Kama unasubiri simu muhimu, usitishwe na SMS ambazo hazina ushahidi.
Lakini pia tumia simu yako kwa busara kuepuka kupata athari za Radio waves
Maelezo zaidi tembelea:NASA  Wikipedia

1 comment:

Popular Posts